• HABARI MPYA

  Monday, January 19, 2015

  TUNISIA NAYO YASHIKWA, 1-1 NA CERPE VERDE AFCON

  TIMU ya taifa ya Tunisia, imetoka sare ya 1-1 na Cape Verde katika mchezo wa Kundi B, Fainali za Mataifa ya Afrika usiku huu Uwanja wa Ebebiyín, Equatorial Guinea.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Eric Arnaud Otogo-Castane, Mohamed Ali Moncer alitangulia kuifungia Tunisia dakika ya 70, kabla ya 
  Heldon Augusto Almeida Ramos kusawazisha kwa penalti dakika ya 77.
  Matokeo hayo yanamaanisha timu zote za Kundi B zinalingana kwa kila kitu baada ya mechi za kwanza Jumapili.
  Mapema Zambia ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 pia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Given Singuluma akitangulia kuifungia Chipolopolo dakika ya pili ya mchezo, kabla ya Yannick Bolasie kuisawazishia DRC dakika ya 66.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TUNISIA NAYO YASHIKWA, 1-1 NA CERPE VERDE AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top