• HABARI MPYA

  Tuesday, January 20, 2015

  ROMARIO 'ANATEMBEA' NA KITOTO KILIKUWA HAKIJAZALIWA WAKATI ANAKUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA 1994

  GWIJI wa soka Brazil, Romario amedhihirisha makali yake si katika kufunga mabao tu uwanjani, bali hata kwa vimwana ni matata vile vile, kufuatia kukichanganya kwa mapenzi kibinti ambacho anakizidi karibu miaka 30.
  Mshindi huyo wa Kombe la Dunia amenasa kwenye penzi la binti wa umri wa miaka 19, mwimbaji wa Kimarekani, Dixie Pratt kiasi cha kuthubutu kuposti picha zao za faragha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa 'wanakula bata' visiwa vya Caribbean, huko Aruba.
  'Mdingi' huyo wa umri wa miaka 48 inafahamika alianza kujiachia na kibinti hicho Oktoba mwaka 2014 baada ya kutengana na mkewe Isabella Bittencourt na ameposti mapicha kibao ya maisha yake na kitoto hicho, ambayo imemsaidia Pratt kuongeza wafuasi wapya 13,000 katika akaunti yake ya Instagram.
  Brazil icon Romario poses for a picture with his 19-year-old girlfriend Dixie Pratt on holiday in Aruba
  Gwiji wa Brazil, Romario akiwa na mpenzi wake, Dixie Pratt wakila bata Aruba

  Pamoja na kwamba Romario anabaki na heshima ya gwiji wa Brazil, anatoka na kabinti anakokazidi miaka 29, ambako halikuwa hata hakajazaliwa wakati mshambuliaji huyo mkubwa anafunga mabao matano kuiwezesha nchi yake kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1994.
  Nyota huyo wa zamani wa Barcelona pia alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa FIFA na Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia katika mwaka huo huo na aliendelea kucheza hadi alipofikisha miaka 40 na zaidi, akiweka rekodi ya mchezaji wa pili kufunga mabao mengi, zaidi ya 1,000 katika historia ya soka duniani (nyuma ya mshambuliaji wa Austrian-Czech, Josef 'Pepi' Bican).
  Romario netted over 1,000 goals and is the second most prolific striker in football history
  Romario alifunga mabao zaidi ya 1,000 na kuweka rekodi ya mchezaji wa pili kufunga mabao zaidi duniani

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2918194/Romario-dating-teenage-beauty-Dixie-Pratt.html#ixzz3POTJLiJW 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROMARIO 'ANATEMBEA' NA KITOTO KILIKUWA HAKIJAZALIWA WAKATI ANAKUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA 1994 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top