• HABARI MPYA

  Sunday, January 11, 2015

  REAL MADRID YAUA 3-0 NA KUZIACHA BARCA, ATLETICO KILELENI LA LIGA

  TIMU ya Real Madrid usiku huu imeshinda mechi yake ya kwanza mwaka 2015 baada ya kuifumua mabao 3-0 Espanyol katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Bernabeu.
  Cristiano Ronaldo amerejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupona maumivu ya goti, lakini akanyimwa pasi na Gareth Bale akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.
  Mfungaji bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez alifunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa pasi nzuri ya Ronaldo, kabla ya winga wa zamani wa Tottenham, Gareth Bale kuwafungia Los Blancos bao la pili kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 28.
  Bale alizomewa na mashabiki Uwanja wa nyumbani kipindi cha pili baada ya kumnyima pasi Ronaldo akiwa kwenye nafasi ya kufunga. Klabu hiyo bingwa wa dunia, ilipata pigo baada ya beki wake, Fabio Coentrao kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Jose Alberto Canas.
  Nacho aliyetokea benchi alihitimisha shangwe za ushindi wa kwanza wa Real 2015 kwa kufunga bao la tatu dakika ya 76 akimalizia krosi maridadi ya Alvaro Arbeloa. 
  Real Madrid sasa inapaa kileleni kwa pointi nne zaidi, dhidi ya mahasimu wake, Barcelona na Atletico Madrid.
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Arbeloa, Pepe, Varane, Coentrao, James/Nacho), Kroos/Khedira), Isco, Bale, Benzema/Illarramendi na Ronaldo. 
  Espanyoll Casilla, Arbilla, Colotto, Alvaro, Fuentes/Casanova, Canas, Joan/Stuani, Sanchez/Conde, Sergio Garcia, Caicedo na Montanes. 
  The Wales international leaps with joy after netting his seventh goal in La Liga this season to give Real a 2-0 lead
  Winga wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale akishangilia baada ya kufunga bao lake la saba katika msimu huu wa La Liga, Real ikishinda 3-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAUA 3-0 NA KUZIACHA BARCA, ATLETICO KILELENI LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top