• HABARI MPYA

  Wednesday, January 21, 2015

  MBWANA SAMATTA AUMIA ENKA AKIWA MAJARIBONI URUSI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta amekosa mechi ya kwanza ya majaribio leo katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi kutokana na maumivu ya enka, kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo.
  CSKA imemualika Mtanzania huyo anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa majaribio, lakini haikumtumia leo ikishinda 1-0 dhidi ya Sion katika mchezo wa kirafiki.
  Bao pekee la ushindi la CSKA leo limefungwa na Eremenko dakika ya 74 na Samatta atakuwa na nafasi nyingine kesho, wakati timu hiyo itakapomenyana na FSV Frankfurt katika mchezo mwingine wa kirafiki.
  Mbwana Samatta yuko CSKA Moscow kwa majaribio
  Mbwana Samatta akiwa mazoezini na timu hiyo juzi
  Mbwana Samatta amevutiwa timu hiyo ya Ulaya
  Samatta aliumia enka na amekosa mchezo wa kirafiki leo

  Samatta aliyekwenda Ulaya mwishoni mwa wiki, awali ilikuwa afanye majaribio Hispania, lakini CSKA ikavutiwa naye na kumuomba iwe naye imtazame.
  Kwa ujumla klabu hiyo imeridhishwa sana na Samatta na ndiyo sababu haina papara za kumtumia akiwa hajisikii vizuri. 
  Mbali na Samatta, wachezaji wengine waliokosa mechi hiyo leo ni George Shennikov, Georgi Milanov, Svetoslav St George na Dmitri Efremov ambao majeruhi pia. 
  Wachezaji wote hao watasafiri hadi Moscow kwa vipimo. 
  Kikosi cha CSKA leo kilikuwa: Akinfeev, Fernandez, V. Berezutski, Ignashevich/Black dk60), Nababkin/Gapon dk46, Wernbloom/Cauna dk46, Nath, Tosic, Eremenko, Dzagoev/Panchenko dk60 na Musa.
  Sion: Vanin, Zhane, Lacroix, Ciss, Ziegler/Ramirez dk78, Vontsak, Ndoye, Fedele/Pare dk78, Akolo, Assifua/Yarti dk70 na Fallon/Wuthrich dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AUMIA ENKA AKIWA MAJARIBONI URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top