• HABARI MPYA

  Saturday, January 17, 2015

  MBEYA CITY YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR KIRUMBA

  BAO pekee la Peter Mapunda dakika ya 80 limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Kwa ushindi huo, Mbeya City wanatimiza pointi 11 baada ya mechi tisa wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 14 baada ya mechi 10.
  Mechi nyingine zilizochezwa leo za Ligi Kuu, Yanga SC imegawana pointi na Ruvu Shooting kwa sare ya 0-0, Azam FC imeshinda 1-0 dhidi ya Stand United, Simba SC imeshinda 2-0 dhidi ya Ndanda FC, wakati Mgambo Shooting imetoka 0-0 na Prisons.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top