// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA YAFANYA MAANGAMIZI ENGLAND, YAITANDIKA SWANSEA 5-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA YAFANYA MAANGAMIZI ENGLAND, YAITANDIKA SWANSEA 5-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, January 17, 2015

    CHELSEA YAFANYA MAANGAMIZI ENGLAND, YAITANDIKA SWANSEA 5-0

    CHELSEA imezinduka na kuichapa maao 5-0 Swansea City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa leo, Uwanja wa Liberty.
    Kiungo Mbrazil Oscar alifungua biashara kwa bao zuri dakika ya kwanza, kabla ya Diego Costa kufunga la pili dakika ya 20 na la tatu dakika ya 34.
    Oscar akafunga tena dakika ya 36 kabla ya nyota wa Ujerumani, Andre Schurrle kukamilisha shangwe za mabao dakika ya 79. 
    Kwa ushindi huo, The Blues ya Jose Mourinho inafikisha pointi 52 baada ya mechi 22 na kujiimarisha kileleni, dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 47 za mechi 21. 
    Kikosi cha Swansea City kilikuwa; Fabianski, Tiendalli, Fernandez, Williams, Taylor, Dyer/Barrow dk74, Carroll, Sigurdsson, Routledge/Emnes dk32, Oliveira/Fulton dk66 na Gomis. 
    Chelsea; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Luis, Matic, Fabregas/Ramires dk74, Willian/Schurrle dk76, Oscar, Hazard na Costa/Remy dk74. 
    The Chelsea players celebrate during the first half - during which they managed to score a remarkable four goals 
    Wachezaji wa Chelsea wakipongezana kwa ushindi wa leo

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2914549/Swansea-City-0-5-Chelsea-Blues-boys-Brazil-batter-Swans-Jose-Mourinho-s-five-points-clear-table.html#ixzz3P6WsDMAl 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAFANYA MAANGAMIZI ENGLAND, YAITANDIKA SWANSEA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top