• HABARI MPYA

  Tuesday, January 13, 2015

  KIPA KUSHINDA BALLON D'OR, MBWA ATAPIGA MSWAKI- MANUEL NEUER

  MLINDA mlango bora zaidi kwa sasa duniani, Mjerumani Manuel Neuer amesema ni vigumu kwa kipa kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or kwa sababu, ambazo haziwezi kubadilika.
  Kipa huyo tegemeo wa Ujerumani na Bayern Munich alishika nafasi ya tatu katika kinyang'anyiro cha cha tuzo hiyo nyuma ya Cristiano Ronaldo aliyeibuka mshindi kwa mara ya pili mfululizo na Lionel Messi aliyekuwa wa pili kama mwaka jana.
  Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu matokeo baada ya tuzo hizo jana mjini Zurich, Usiwsi, Neuer alisema; "Wakati wote nilijua itakuwa vigumu kuwashinda washambuliaji,".
  Bayern Munich and Germany goalkeeper Manuel Neuer failed to win the Ballon d'Or on Monday evening
  Kipa wa Bayern Munich na Ujerumani, Manuel Neuer amekosa tuzo ya Ballon d'Or jana usiku

  "Cristiano Ronaldo na Lionel Messi waliweka alama zao katika dunia ya soka mwaka jana. Kama kipa, ni vigumu mno kufanya hivyo.
  "Wakati unapowadia mchezo wa soka, kitu cha kwanza ambacho mtu yeyote anauliza ni nani amefunga mabao na si kuhusu kipa amechezaje. Sifikirii kama itabadilika,".
  Hata hivyo, Neuer alitajwa kuwa kipa wa kikosi bora cha mwaka duniani cha FIFA, baada ya kuisaidia Bayern kutwaa taji la Bundesliga na kuipa Ujerumani Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA KUSHINDA BALLON D'OR, MBWA ATAPIGA MSWAKI- MANUEL NEUER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top