• HABARI MPYA

  Friday, January 02, 2015

  JAVU AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUJERUHIWA ‘TAYA’ ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Hussein Javu alikimbizwa hospitali mwishoni mwa mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa ya Jang’ombe baada ya kuumia.
  Javu alitokea benchi dakika ya 65 kwenda kuchukua nafasi ya Mbrazil, Andrey Coutinho lakini baada ya dakika 20 akaumia na kutibiwa kwa dakika mbili kabla ya kupakizwa kwenye gari kukimbizwa hospitali.
  Javu alipigwa daluga la sehemu ya mdomoni (taya) na mchezaji wa Taifa na kuumia, hivyo nafasi yake akaingia Rajab Zahir dakika ya 86 kumalizia mchezo.
  Daktari wa Yanga SC, Sufiani Juma kulia na kiungo Nizar Khalfan wakimsindikiza hospitali Javu aliyelala kwenye gari

  Daktari wa Yanga SC, Sufiani Juma aliongozana na kiungo Nizar Khalfan kumkimbiza Javu hospitali ya A l Haramain katika gari maalum la wagonjwa lililokuwapo Uwanja wa Amaan.
  Kufika huko akafanyiwa vipimo na uchunguzi zaidi ikaonekana hakuna madhara makubwa, ingawa mchezaji mwenyewe alikuwa analalamika kuhisi maumivu makali. 
  Pamoja na hayo, Javu alipatiwa dawa za maumivu na kurejea kambini. 
  Yanga SC ilishinda mabao 4-0 katika mchezo huo, winga Simon Msuva akifunga matatu na kumsetia moja Mliberia, Kpah Sherman kufunga la nne.   
  Javu akichezewa rafu na beki wa Taifa katika mchezo huo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JAVU AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUJERUHIWA ‘TAYA’ ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top