• HABARI MPYA

  Sunday, January 18, 2015

  GABON YAANZA VYEMA AFCON, YAICHAPA 2-0 BURKINA FASO

  GABON imepanda kileleni mwa Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso Uwanja wa Bata usiku wa Jumamosi.
  Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang, aliifungia Gabon bao la kwanza dakika ya 19, kabla ya Malick Evouna kufunga la pili dakika ya 72.
  Gabon sasa inaanza na pointi tatu kileleni mwa kundi, mbele ya wenyeji Equatorial Guinea wenye pointi moja sawa na Kongo baada ya sare ya 1-1 baina yao, wakati Burkina Fasso inashika mkia ikiwa haina pointi.

  Katika mchezo uliotagulia, bao la dakika ya 87 la Bifouma Koulossa liliinusuru Kongo kulala mbele ya wenyeji Equatorial Guinea.  
  Nsue Lopez alitangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 16 na ilibaki kidogo Equatorial Guinea waanze na ushindi.
  Mechi ijayo, Equatorial Guinea watamenyana na Burkina Faso, wakati Kongo itaivaa Gabon mjini Bata Januari 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GABON YAANZA VYEMA AFCON, YAICHAPA 2-0 BURKINA FASO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top