• HABARI MPYA

  Friday, January 02, 2015

  ENYEAMA KIPA BORA UFARANSA

  Na Mwandishi Wetu, LAGOS
  KIPA wa kimataifa wa Nigeria, Vincent Enyeama amateuliwa tena kuwa kipa bora wa Ligi Kuu ya Ufaransa, maarufu Ligue 1 mwaka 2014 na gazeti la L’Equipe la nchini humo.
  Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32 ameteuliwa kipa bora wa 2014 licha ya klabu yake kuanza vibaya msimu wa 2014-2015, ambao unaifanya timu hiyo ishike nafasi ya 13 katika ligi ya timu 20.
  Enyeama amecheza dakika zote katika mechi 56 za Lille kwenye ligi, tangu arejee kutoka Maccabi Tel Aviv ya Israel mwaka 2013 alipokuwa anacheza kwa mkopo.
  Huu ni mwaka wa pili mfululizo Enyeama anachaguliwa kipa bora wa Ligue 1 na gazeti la L’Equipe.
  Vincent Enyema kwa mara ya pili mfululizo ameteuliwa kipa bora Ufaransa

  Kipa wa zamani wa Super Eagles, Ike Shorunmu alicheza na Enyeama timu ya taifa ya Nigeria na hastaajabu mafanikio ya mlinda mwenzake huyo wa zamani timu ya nchi.
  Wachezaji wengine watatu kutoka washindi wa mwaka jana wamerudi tena katika tuzo za mwaka huu, ambao ni Gregory Van der Wiel, Maxwell na Zlatan Ibrahimovic.
  Simon Kjaer ni mchezaji mwingine pekee wa LOSC Lille kuingia kwenye orodha hiyo, wakati beki wa Olympic Marseille, Mcameroon, Nicolas N’koulou ndiye mchezaji mwingine kuteuliwa na jarida la L’Equipe.
  Kikosi kamili cha L’Equipe XI ni; Makipa; Vincent Enyeama (Nigeria / LOSC Lille), mabeki; Gregory Van der Wiel (The Netherlands / PSG), Simon Kjaer (Denmark / LOSC Lille), Nicolas N’koulou (Cameroun / Marseille), Maxwell (Brazil / PSG).
  Viungo; Georges Ntep (France/ Rennes), Marco Verratti (Italy / PSG), Jeremy Toulalan (France/ Monaco), Javier Pastore (Argentina / PSG) na washambuliaji Zlatan Ibrahimovic (SWE / Paris SG) na Lacazette (FRA / Lyon).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENYEAMA KIPA BORA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top