• HABARI MPYA

  Friday, January 02, 2015

  AZAM FC YAWAKAZIA MABINGWA WATETEZI MAPINDUZI, SARE 2-2 NA KCAA

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na KCCA ya Uganda katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Matokeo hayo, yanafanya timu zote za Kundi hilo zianze kwa pointi moja, baada ya mchezo wa awali baina ya Mtende FC na KMKM kumalizika kwa sare ya bila kufungana Amaan. 
  Hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwao bao 1-0 lililofungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya 38.
  Bocco alifunga bao lake la pili katika mechi mbili mfululizo alizocheza baada ya kuwa nje tangu Agosti mwaka huu maumivu, akimalizia krosi ya Mganda Brian Majwega. Awali alifunga katika sare ya 2-2 na Yanga SC mechi ya Ligi Kuu.
  John Bocco akipiga shuti kuifungia Azam FC bao la kwanza leo
  Himid Mao akimtoka Nahodha wa KCCA, Mpiima Saka

  Hata hivyo, mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi, KCCA waliingia na kasi nzuri kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 49, lililofungwa na William Waori kwa shuti la umbali wa mita 22.
  Baada ya bao hilo, mchezo ulichangamka zaidi, kila timu ikisaka bao la ushindi na walikuwa na Azam FC waliopata bao la pili dakika ya 53 mfungaji Nahodha Msaidizi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Majwega.
  KCCA ilisawazisha bao hilo dakika ya 73 kupitia kwa Tom Masiko aliyepiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja nyavuni, baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Erasto Nyoni.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Himid Mao/Kelvin Friday dk75, Salum Abubakar, John Bocco/Gaudence Mwaikimba dk89, Amri Kiemba/Waziri Salum dk39 na Brian Majwega.
  KCCA; Emmanuel Opio, Mpiima Saka, Simon Nawanja, Ronnie Kuseka, Ibrahim Kiiza, Hakim Senkumba, Tom Masiko, Owen Kasuule/Paul Macureez dk46, Herman Wasswa/Derick Ndisambi dk72, William Waori na Simon Mbazipa/Yassin Magume dk72.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWAKAZIA MABINGWA WATETEZI MAPINDUZI, SARE 2-2 NA KCAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top