• HABARI MPYA

  Friday, January 09, 2015

  BARCELONA WAFANYA MAUAJI HISPANIA, WAPIGA MTU 5-0

  BARCELONA imefanya mauaji katika Kombe la Mfalme, baada ya kuifumua Elche mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Uwanja wa Camp Nou usiku huu.
  Na wauaji wenyewe ni Neymar aliyefunga mabao mawili, Lionel Messi, Luis Suarez na Jordi Alba waliofunga bao moja kila mmoja katika ushindi huo mnono.
  Ushindi huo unarejesha hali ya kujiamini ndani ya kikosi cha Luis Enrique kuelekea mchezo wa marudiano, wakitoka kufungwa na timu ya kocha David Moyes, Real Sociedad kwenye mechi yao iliyopita. 
  Elche imeshinda mechi moja tu kati ya 10 kwenye mashindano yote msimu huu na sasa inachungulia mlango wa kutokea Kombe la Mfalme.
  Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Alves, Pique/Samper dk75, Alba/Correira dk60, Bartra, Mascherano, Rakitic, Roberto, Messi, Suarez na Neymar/Pedro dk66. 
  Elche; Tyton, Cisma/Fragapane dk72, Lomban, Suarez, Albacar, Pelegrin, Roco, Fajr, Pasalic, Coro/Jonathas dk57 na Herrera/Niguez dk63.
  Barcelona got back to winning ways against Elche on Thursday evening after their disappointing defeat to Real Sociedad
  Wachezaji wa Barcelona wakipongezana kwa ushindi wao dhidi ya Elche usiku wa Alhamisi 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2902565/Barcelona-5-0-Elche-Lionel-Messi-Luis-Suarez-Neymar-score-Luis-Enrique-s-triumph-Copa-del-Rey-clash.html#ixzz3OH7PDszo 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA WAFANYA MAUAJI HISPANIA, WAPIGA MTU 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top