Kikosi cha Prisons |
Na Prince Akbar
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya mechi
kadhaa za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kutokea dharura, hivyo
kushindwa kufanyika kwa mujibu wa kanuni.
Taarifa kutoka TFF, zimesema kwamba sababu za mabadiliko hayo
ni timu ya Tanzania Prisons kupata ajali wakati ikienda Tanga kwa ajili ya
mechi dhidi ya Mgambo Shooting na mvua kubwa iliyonyesha mjini Mwanza na kusababisha kutofanyika kwa mechi ya Oktoba
31 mwaka huu kati ya Toto Africans na Kagera Sugar.
Sasa Mgambo Shooting na Tanzania Prisons zitamenyana Novemba 14
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shooting na Prisons Novemba 18, Uwanja wa Mabatini,
Mlandizi mkoani Pwani, Mtibwa Sugar na JKT Ruvu Novemba 7 Uwanja wa Manungu,
Morogoro, Kagera Sugar na Prisons Novemba 4 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na Ruvu
Shooting na Toto Africans siku hiyo Mabatini, Pwani.
Mabadiliko hayo ya mechi za Ligi Kuu yameingilia hadi mechi
za Ligi Daraja la Kwanza na sasa Tessema na Ndanda waliokuwa wamenyane Novemba 4,
Uwanja wa Mabatini, watacheza Novemba 5 katika uwanja huo huo.
Mabadiliko hayo yanaipisha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati
ya Ruvu Shooting na Toto Africans ambayo itachezwa Novemba 4, kwenye uwanja huo
huo.
Ashanti United na Tessema zilizokuwa zicheze Uwanja wa
Mabatini Novemba 7, sasa zitacheza siku inayofuata, Novemba. Mabadiliko hayo ni
kutoa fursa ya kupumzika kwa Tessema ambayo Novemba 5 itacheza na Ndanda.