• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 24, 2012

  ALHAJ MANJI HII SIYO MAGUMASHI KAMA YA ALHAJ RAGE?

  Mwenyekiti wa Yanga, Alhaj Yussuf Mehboob Manji (kulia) akisaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Uwanja wa Kaunda na Mkurugenzi wa Kampuni ya Beijing Construtcions ya China, walioujenga Uwanja wa Taifa pia, Geng Hijuan jana makao makuu ya Yanga, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage alisaini pia mkataba na Waturuki mwaka jana kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa klabu yake, lakini hadi sasa hakuna hata dalili za ujenzi huo, je, mkataba huu wa Manji na Wachina hautakuwa 'porojo' kama wa Rage na Waturuki? Bila shaka ni jambo la kusubiri na kuona. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ALHAJ MANJI HII SIYO MAGUMASHI KAMA YA ALHAJ RAGE? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top