• HABARI MPYA

    Tuesday, November 20, 2012

    YAW BERKO BADO YUPO YUPO SANA YANGA SC


    Yaw Berko
    Na Mahmoud Zubeiry
    KIPA Mghana, Yaw Berko hataachwa katika klabu ya Yanga kama ambavyo magazeti mengi nchini yamekuwa yakiandika.
    Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba Berko ambaye mkataba wake unamalizika Mei mwakani, ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba huo.
    Kipa huyo anayelipwa mshahara wa Sh. Milioni 1.5 kwa mwezi, amerudishwa benchi siku za karibuni baada ya kufululiza kufungwa mabao rahisi, jambo ambalo lilimkera kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
    Kwa sababu hiyo, vyombo vya habari vikaanza kubashiri kwamba ataachwa mwezi ujao kwa sababu pia, tayari klabu hiyo imesajili mchezaji mwingine wa kigeni, Kabange Twite kutoka APR ya Rwanda.
    Kanuni za Usajili za Ligi Kuu zinataka wachezaji watano tu wa kigeni kwa kila klabu, na Yanga tayari inao Yaw Berko, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Hamisi Kiiza kutoka Uganda na Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
    Lakini habari zaidi zinasema Kabange atachukua nafasi moja kati ya mbili zinazotarajiwa kuachwa na wachezaji wawili wa klabu hiyo, ambao watauzwa hivi karibuni, Niyonzima na Kavumbangu. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YAW BERKO BADO YUPO YUPO SANA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top