• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 25, 2012

  BURUNDI WAIPIGA KHAMSA SOMALIA TUSKER CHALLENGE

  Wachezaji wa Burundi, wakimpongeza Chris Nduwarugira baada ya kufunga katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Somalia Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda. Katika mchezo huo, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BURUNDI WAIPIGA KHAMSA SOMALIA TUSKER CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top