• HABARI MPYA

    Saturday, November 24, 2012

    SIMBA YAFUNIKA MBAYA TUSKER CHALLENGE 2012

    Mwinyi Kazimoto, mmoja wa wachezaji wanaoiwakilisha Simba katika Tusker Challenge 2012

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wanaongoza kuwa na wachezaji wengi katika Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, Tusker Challenge 2012 inayoanza leo mjini hapa, wakiwa na jumla ya wachezaji 10, yaani kasoro mmoja tu kuunda kikosi kamili cha kwanza.
    Wachezaji wa Simba waliopo hapa na timu zao kwenye mabano ni Nassor Masoud 'Cholo' (Zanzibar), Juma Kaseja (Bara), Shomari Kapombe (Bara), Amir Maftah (Bara), Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi Kazimoto (Bara), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Bara), Mrisho Ngassa (Bara), Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).
    Simba wenye maskani yao pale Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam wanafuatiwa na Azam FC ya Chamazi, kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye mashindano haya yanayofunguliwa leo na rais wa Shirkisho la Soa Afrika (CAF), Issa Hayatou Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, Kampala.
    Wachezaji wa Simba na timu zao kwenye mabano ni Nassor Masoud 'Cholo' (Zanzibar), Juma Kaseja (Bara), Shomari Kapombe (Bara) na Amir Maftah (Bara), Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi Kazimoto (Bara), Ramadhan Singano ‘Messi’ (Bara), Mrisho Ngassa (Bara), Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).
    Wachezaji wa Azam waliopo hapa na timu zao kwenye mabano ni Mwadini Ali (Zanzibar), Samir Haji Nuhu (Zanzibar), Aggrey Morris (Zanzibar), Abdulhalim Humud (Zanzibar), Khamis Mcha 'Vialli' (Zanzibar) ,Deogratius Munishi ‘Dida’ (Bara), Erasto Nyoni (Bara), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Bara) na John Bocco ‘Adebayor’ (Bara).
    Azam yenye wachezaji tisa, inafuatiwa na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC wenye wachezaji wanane, wakati klabu nyingin za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zenye wachezaji Challenge ni Mtibwa Sugar ya Morogoro watatu, JKT Oljoro ya Arusha mmoja sawa na Coastal Union ya Tanga.
    Yanga inawakilishwa na Nadir Haroub Ali 'Canavaro'(Zanzibar), Didier Kavumbangu (Burundi), Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda), Kevin Yondan (Bara), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Bara), Frank Domayo (Bara) na Simon Msuva (Bara), wakati Mtibwa Sugar ni Twaha Mohammed (Zanzibar), Issa Rashid (Bara) na Shaaban Nditi (Bara).
    Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka Arusha, JKT Oljoro wao wanawakilishwa na Amir Hamad aliye na kikosi cha Zanzibar, wakati Wagosi wa Kaya, Coastal Union wanawakilishwa na Suleiman Kassim 'Selembe' aliye na Zanzibar pia.

    LIGI KUU BARA INAVYOWAKILKISHWA CHALLENGE:
    Simba (10); Nassor Masoud 'Cholo' (Zanzibar), Juma Kaseja (Bara), Shomari Kapombe (Bara) na Amir Maftah (Bara), Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi Kazimoto (Bara), Ramadhan Singano ‘Messi’ (Bara), Mrisho Ngassa (Bara), Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).

    Azam (9); Mwadini Ali (Zanzibar), Salmin Haji Nuhu(Zanzibar), Agrey Moris(Zanzibar), Abdulhalim Humoud(Zanzibar), Khamis Mcha Khamis 'Viali'(Zanzibar) ,Deogratius Mushi ‘Dida’ (Bara), Erasto Nyoni (Bara), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Bara), John Bocco ‘Adebayor’ (Bara).

    Yanga (8); Nadir Haroub Ali 'Canavaro'(Zanzibar), Didier Kavumbangu (Burundi), Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda), Kevin Yondan (Bara), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Bara), Frank Domayo (Bara), Simon Msuva (Bara).

    Mtibwa Sugar(3); Twaha Mohammed (Zanzibar), Issa Rashid (Bara), Shaaban Nditi (Bara)

    JKT oljoro(1); Amir Hamad (Zanzibar)

    Coastal Union(1); Suleiman Kassim 'Selembe' (Zanzibar)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA YAFUNIKA MBAYA TUSKER CHALLENGE 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top