• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 27, 2012

  MECHI SITA MABAO 12 NAMBOOLE


  John Bocco kushoto
  Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
  KATIKA mechi sita za awali za makundi yote kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Tusker Challenge hadi jana jumla ya mabao 12 yamefungwa.
  Baada ya kila timu kushuka dimbani mara moja, Burundi ndiyo wameweza kuvuna mabao mengi katika mechi moja, matano wakifuatiwa na Tanzania Bara na Rwanda, waliovuna mabao mawili kila mmoja.
  Mshambuliaji wa Tanzania John Bocco anachuana kwa ufungaji na washambuliaji wa Burundi, Chris Nduwarugira na Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
  Wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna Niyonzima na Jean Mugiraneza.
  Bocco ana nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
  Lakini Bocco kama atacheza kwa kiwango cha jana, anaweza akawa mwiba hata mbele ya Burundi Novemba 28.
  Kwa sasa Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC) kuzuiliwa na klabu yao.

  WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
  John Bocco                     Tanzania 2
  Yussuf Ndikumana          Burundi   2
  Suleiman Ndikumana      Burundi   2
  Yussuf Ndikumana          Burundi   1
  Mohamed Jabril              Somalia   1(penalti).
  Geoffrey Kizito                Uganda    1
  Yonatal Teklemariam      Ethiopia   1
  Haruna Niyonzima          Rwanda   1
  Jean Mugiraneza            Rwanda   1
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MECHI SITA MABAO 12 NAMBOOLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top