• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 27, 2012

  SHARO MILIONEA KUZIKWA LEO TANGA

  MSANII Hussein Ramadhani Mkiete anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao, Tanga.
  Kwa mujibu wa Diwani Makame Seif ambaye ni rafiki wa karibu marehemu, aliyefarfiki kwa ajali Saa 2:00 usiku jana eneo la Maguzoni Tanga, Polisi wametambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi.
  Diwani huyu amemfahamisha mwandishi kuwa Sharo Millionea ameumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono. Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba itatolewa. Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo imeshafika Hospitali ya Teule ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SHARO MILIONEA KUZIKWA LEO TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top