• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 24, 2012

  BENITEZ AWATIMUA LAMPARD, COLE BAADA YA KIKAO CHA SAA TATU NA ABRAMOVICH


  MAGWIJI wa Chelsea, Frank Lampard na Ashley Cole wataondoka mwishoni mwa msimu baada ya Rafa Benitez kuthibitisha kubomoka kwa kikosi cha ubingwa cha Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Wachezaji wote hao wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu na kocha mpya wa Chelsea amesema hawastahili kuendelea kubaki Stamford Bridge baada ya msimu huu.
  Lampard, mfungaji bora namba tatu wa kihistoria wa Chelsea, ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England, manne ya FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika miaka yake 11 ndani ya klabu hiyo.
  Going: Ashley Cole and Frank Lampard (below) will be allowed to leave Chelsea
  Safari: Ashley Cole na Frank Lampard (chini) watatemwa Chelsea
  Legend: Frank Lampard
  Cole, aliyejiunga na Chelsea akitokea Arsenal mwaka 2006, ameshinda taji la Ligi Kuu ya England, manne ya FA na Ligi ya Mabingwa kwa kipindi chake cha kuishi Stamford Bridge.
  Benitez alionekana kwenye picha na Mkurugenzi wa Ufundi, Michael Emenalo wakiwa kwenye chakula cha usiku na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.
  "Nilitumia saa kama mbili au tatu na mmiliki, tulizungumzia kila kitu. Anafahamu mawazo yangu, lakini hatukuwa na muda wa kutosha pamoja. Labda wakati mwingine tena.
  "Kama unajiamini na kujieleza, kila mmoja anaweza kukuelewa. Mtazamo wangu kwa mmiliki, ni mtu mzuri. Unaweza kuzungumza naye na ni mwelewa. Anapenda kuona una mawazo mazuri
  Short term: Rafa Benitez still plans to use the players until their contracts are up
  Mipango ya muda mfupi: Rafa Benitez anataka kuendelea na wachezaji waliopo Chelsea hadi mwisho wa mikataba yao
  Not just Torres: Benitez wants to improve the whole team
  Si Torres pekee: Benitez anataka kuiboresha timu nzima

  Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2237633/Frank-Lampard-Ashley-Cole-leave-says-Rafa-Benitez.html#ixzz2D6wWWLeM 
  Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BENITEZ AWATIMUA LAMPARD, COLE BAADA YA KIKAO CHA SAA TATU NA ABRAMOVICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top