• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 27, 2012

  KIBOKO YA SIMBA, YANGA ATUA AZAM FC


  Seif Abdallah
  Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
  MSHAMBULIAJI wa Ruvu Shooting, Seif Abdallah amethibitisha kwamba kuanzia Januari mwakani atakuwa akichezea Azam FC ya Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Seif ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu akiwa na Ruvu Shooting, aliiambia BIN ZUBEIRY jana mjini hapa kwamba amekwishafikia makubaliano na Azam kujiunga nao mwakani.
  “Azam ni timu kubwa, nitafurahi sana kuanza kuichezea mwakani, naamini ni hatua moja mbele ya mafanikio katika maisha yangu ya mpira na ninaamini pia nitafanya vizuri kwa sababu najiamini,”alisema chipukizi huyo.
  Seif ana mabao saba hadi baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, akiwa anachuana na Didier Kavumbangu wa Yanga na Kipre Tcheche wa Azam, ambao kila mmoja ana mabao nane. 
  Seif, ambaye katika CECAFA Tusker Challenge anaichezea Zanzibar alizifunga timu zote kubwa katika mzunguko wa kwanza, Simba, Yanga na Azam na baada ya hapo, vigogo wote hao wakawa wanamuwinda.
  Yanga walifanya jitihada, wakati Simba walikuwa wanasikilizia, lakini Azam imewapiku wote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIBOKO YA SIMBA, YANGA ATUA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top