• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 30, 2012

  WATU WANA HAMU NA CHUJI ILE MBAYA

  Mashabiki wa Tanzania waliokuja mjini hapa kuishangilia timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars, wana hamu sana ya kumuona kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ anacheza katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge. Kiungu huyu hajapangwa katika mechi hata moja kati ya mbili za awali za Bara, Kilimanjaro Stars, dhidi ya Sudan na Burundi. Kocha Mdenmark, Kim Poulsen alimuinua mara katika mechi ya kwanza na Sudan wakati Frank Domayo alipoumia, lakini kiungo huyo chipukiziwa Yanga aliponuka na kuendelea Chuji aliendelea kuishi ‘benchi’. Kesho Stars itacheza mechi ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Somalia, je Kim atampa nafasi kiungo huyo wa Yanga pia, ambaye kwa sasa utambulisho wake mpya ni mzuzu? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WATU WANA HAMU NA CHUJI ILE MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top