• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 28, 2012

  STARS KAMBINI DAR BAADA YA CHALLENGE

  Kim Poulsen akijadiliana jambo na msaidizi wake, Sylvester Marsh Uwanja wa Namboole jana

  Na Boniface Wambura, Kampala
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kuingia kambini baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inayoendelea Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda hadi Desemba 8 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, ambaye anakiongoza kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kwenye mashindano haya, Stars itaingia kambini kujiandaa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia, Chipolopolo itakayochezwa Desemba 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Baada ya pambano dhidi ya Chipolopolo, wachezaji watapata mapumziko ya wiki mbili kabla ya kuingia tena kambini Januari 6 hadi 20 mwakani kwa ajili ya mechi nyingine za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.
  Kim anatarajia kuongeza kipa mmoja kwenye kikosi chake ili kuwasaidia Nahodha Juma Kaseja na Deogratias Munishi pamoja na chipukizi kadhaa kutoka timu za taifa za vijana za Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys.
  Vilevile Kim anafuatilia wachezaji wengine kwenye timu ya Zanzibar, Zanzibar Heroes waliopo kwenye Tusker Challenge pia katika kundi C pamoja na timu za Eritrea, Malawi na Rwanda
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: STARS KAMBINI DAR BAADA YA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top