• HABARI MPYA

    Tuesday, November 20, 2012

    MWANASOKA BORA TANZANIA KUPATIKANA DESEMBA 30

    Athimani Iddi 'Chuji' wa Yanga kulia akiwa katika moja ya mechi za Ligi Kuu dhidi ya Mgambo JKT. Je, ataingia kwenye orodha ya wachezaji wa kuwanai tuzo ya Mwanasoka Bora Tanzania?

    Na Prince Akbar
    FAINALI ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka Tanzania, zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo Bright Media zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu mjini Dar es Salaam katika sehemu, ambayo itatangazwa baadaye.
    Mratibu wa mchakato huo, Ahadi Kakore ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mchakato wake ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na mashabiki kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book, Twitter na Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba maalum.
    Amesema kwa sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na  mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza kuonekana ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.
    Amesema kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye fainali watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na maisha ya baadaye baada ya kustaafu.
    Amesema sababu za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni masikini.
    Kakore amesema kwenye semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na fedha ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi wachezaji hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.
    Amesema semina hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na  20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam. Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na  utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa wachezaji pekee. Amesema mshindi wa tunzo hiyo anatarajiwa kupata tuzo, fedha taslim, medali na cheti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MWANASOKA BORA TANZANIA KUPATIKANA DESEMBA 30 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top