• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 27, 2012

  WILSHERE KUONGEZEWA MSHAHARA NA UNAHODHA JUU ARSENAL


  KIUNGO Jack Wilshere yuko mbioni kupewa mkataba mpya wakati kocha Arsene Wenger akijiandaa kumpa beji ya Unahodha wa Arsenal mchezaji huyo.
  Mjadala unaoendelea utamfanya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 aongezewe mshahara wake wa pauni 50,000 kwa wiki anaolipwa.
  Nyota huyo wa England bado ana miaka miwili na nusu katika mkataba wake, lakini Arsenal inataka kumtia pingu ili asiote mbawa.
  Perfect 10: Jack Wilshere was honoured by the famous shirt in the summer
  Jack Wilshere sasa anavaa jezi namba 10
   
  Mshambuliaji Mjerumani, Lukas Podolski ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi kwa sasa Arsenal, pauni 90,000 kwa wiki, na mshahara mpya wa Wilshere unatarajiwa kuwa katika kiwango hicho.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WILSHERE KUONGEZEWA MSHAHARA NA UNAHODHA JUU ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top