• HABARI MPYA

    Saturday, November 10, 2012

    SIMBA B WAINGIA MITINI TAIFA

    MABINGWA wa Kombe la BancABC Sup8R, timu ya vijana ya Simba, maarufu kama Simba B, wameshindwa kutokea uwanjani jioni hii kucheza mchezo wa utangulizi kabla ya kuanza kwa mechi ya kaka zao, Simba A ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Kocha Mkuu wa Simba B, Suleiman Matola amesema kwamba tatizo lipo kwa uongozi wa klabu hiyo, kwani kwa wiki nzima, timu hiyo haijafanya mazoezi kutokana na viongozi kushindwa kuyawezesha.
    Lakini habari zaidi kutoka ndani ya Simba, zinasema kwamba timu hiyo imekwama kwa sasa kwa sababu aliyekuwa anaihudumia, Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameamua kujitenga.
    Inadaiwa Kaburu ametofautiana na viongozi wenzake na yeye ameamua kukaa kando, jambo ambalo limechangia mambo mengi yaende shaghalabagala Simba SC.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA B WAINGIA MITINI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top