Nemanja Vidic hatacheza hawon't play again until December
NAHODHA wa Manchester United, Nemanja Vidic anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja hadi mwishoni mwa mwaka.
Kocha wa United, Sir Alex Ferguson amesema hakutarajia kama beki wake huyo wa kati atakaa nje ya Uwanja hadi Desemba.
Baada ya kupona maumivu makubwa mguu mwaka jana wakitolewa na Basel katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mserbia huyo ameumia tena goti ambalo linahitaji upasuaji.
"Nafikiri tunazungumzia Desemba kuhusu Vidic kupona,' alisema Ferguson. "Labda wakati wa Krisimasi" aliongeza.