• HABARI MPYA

    Sunday, April 01, 2012

    MOURINHO AWATOLEA MBAVUNI MAN CITY

    Mourinho
    KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amekanusha taarifa kwamba amefanya mazungumzo na Manchester City juu ya kujiunga na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England.
    Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari juzi, Mourinho baada ya kuulizwa kuhusu tetesi za kuondoka kwake Santiago Bernabeu mwishoni mwa msimu, kwamba atahamia kwa matajiri City, Mourinho alisema: "Sihitaji kuzungumzia juu ya kuendelea. Nina miaka miwili bado katika mkataba wangu ni sijawahi kusema sitabaki."
    Mshindi huyo wa taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili, baadaye alilazimishwa kukanusha habari juu ya uhusiano wake mbaya na kipa chaguo la kwanza la timu yake, Iker Casillasambao umekuwa mbovu zaidi msimu huu.
    "Hakuna tatizo na Casillas," alisema. "Sina tatizo naye."
    "Baada ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona msimu uliopita, tulifungua mioyo yetu na tuliua tofauti zetu. Kwenye Copa del Rey kadhalika, ,"alisema.
    Mourinho pia aliulizwa kuhusu Zinedine Zidanekusema kwamba angependa kuwa kocha baadaye, lakini akasema, "Unatakiwa kumuuliza mwenyewe juu ya hilo."
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOURINHO AWATOLEA MBAVUNI MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top