• HABARI MPYA

    Wednesday, August 02, 2017

    YANGA NA SINGIDA YARUDISHWA NYUMA SIKU MOJA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHEZO wa kirafiki kati ya Yanga na Singida United uliopangwa kufanyika Agosti 6, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umerudishwa nyuma kwa siku moja kupisha shughuli maalum ya Kiserikali siku hiyo na sasa utafanyika Jumamosi ya Agosti 5.
    Yanga inatarajiwa na kumenyana na Singida United inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Mholanzi Hans van der Pluijm katika mchezo maalum wa kila timu kujaribu kikosi chake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Na kwa sasa kikosi cha kocha Mzambia, George Lwandamina kipo mjini Morogoro kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya, wakianza na mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya mahasimu, Simba, Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa.
    Mashabiki wa Yanga watamuona Ibrahim Hajib kwa mara ya kwanza akiichezea timu yao Jumamosi Uwanja wa Taifa
    Singida United imerejea Ligi Kuu msimu huu tangu iliposhuka mwaka 2002, lakini baada ya kupanda imefanya usajili wa gharama kubwa, ikichukua wachezaji wenye uzoefu mkubwa kutokaa timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
    Maana yake si tu wanatarajiwa kutoa upinzani kwa Yanga Agosri 5, bali pia wanatarajiwa kuwa tishio katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA SINGIDA YARUDISHWA NYUMA SIKU MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top