• HABARI MPYA

  Monday, May 15, 2017

  SAMATTA AGONGA MWANZO MWISHO, GENK YAMPA MTU 2-0 KWAKE

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza vizuri kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikishinda 2-0 ugenini dhidi ya Royal Excel Mouscron Uwanja wa Le Canonnier mjini Mouscron, Ubelgiji kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.
  Mabao ya KRC Genk jana yalifungwa na kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 63 na kiungo Mholanzi, Jean-Paul Boetius dakika ya 70.
  Mbwana Samatta akishughulika katika mchezo wa jana
  Samatta alianza katika mchezo huo na akawa sehemu ya ushindi huo unaoifanya Genk iendelee kuongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League mwakani kwa kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi nane na Samatta jana ameichezea Genk mechi ya 57 tangu ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 19.
  Kati ya mechi hizo 57, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 39 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 35 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 25 msimu huu.
  Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.
  Kikosi cha R.E. Moeskroen kilikuwa; Delac, Manea, Olinga, Trezeguet, Stojanovic, Vojvoda/Debaisieux dk72, Huyghebaert, Peyre, Van Durmen/Selak dk76, Arslanagic na Matulevicius/Kabasele dk64.
  KRC Genk : Ryan, Nastic, Brabec, Dewaest/Janssens dk83, Castagne, Berge, Malinovskyi/Heynen dk63, Schrijvers, Boëtius, Buffel/Naranjo dk63 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AGONGA MWANZO MWISHO, GENK YAMPA MTU 2-0 KWAKE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top