• HABARI MPYA

  Thursday, February 16, 2017

  MBEYA CITY WAJIFICHA KAHAMA KWA AJILI YA STAND UNITED

  Na Mwandishi Wetu, KAHAMA
  KIKOSI cha Mbeya City Fc kimeweka kambi Kahama tangu juzi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Stand United kesho Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Mbeya City imejificha Kahama ikitokea Mwadui, ambako mwishoni mwa wiki ilifungwa 3-2 na wenyeji, Mwadui FC katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu na sasa wanalekekeza nguvu zao kwenye mchezo wa kesho. 
  Mchezaji nyota wa Mbeya City, Mrisho Ngassa kesho anatarajiwa kuisaidia timu yake dhidi ya Stand United

  Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Mohamed Kijuso alisema jana kwamba  kulikuwa na makosa kadhaa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC jambo lililosababisha  kufungwa mabao mawili ya haraka haraka na hatimaye kumaliza dakika 90 City  ikiwa imepoteza mchezo huo wa ugenini kwa bao 3-2.
  "Kwa vyovyote tunalazimika kusaka matokeo kwenye mchezo ujao, tulikuwa na makosa mengi mchezo uliopita, tumesafiri mpaka hapa Kahama kuweka kambi ya siku nne lengo letu likiwa ni kupata utulivu wa kujiandaa vizuri na mchezo wa Ijumaa dhidi ya Stand United,"alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAJIFICHA KAHAMA KWA AJILI YA STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top