• HABARI MPYA

  Tuesday, February 14, 2017

  HAKUNA REFA HATA MMOJA WA TANZANIA FAINALI ZA U-20 AFRIKA

  HAKUNA refa hata mmoja wa Tanzania katika orodha ya marefa 12 walioteuliwa kuchezesha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 nchini Zambia baadaye mwaka huu.
  Kana kwamba hiyo haitoshi, hata katika orodha ya washika vibendera 14 walioteuliwa kuchezesha michuano hiyo ya Total U-20 AFCON Zambia 2017 hakuna Mtanzania pia.
  Fainali za AFCON ya U-20 zinatarajiwa kufanyika Zambia kuanzia Februari 26 hadi Machi 12 katika miji ya Lusaka na Ndola.
  Na kwa mara nyingine Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetuthibitishia kwamba marefa wa Tanzania ni bomu kwa kutoteua hata mmoja kwa ajili ya AFCON ya U-20.
  Marefa waliiteuliwa ni Martins De Carvalho wa Angola mwenye umri wa miaka 39, Zio Juste Ephrem wa Burkina Faso miaka 38, Thierry Nkurunziza wa Burundi miaka 31, Antoine Max Effa Essouma wa Cameroon miaka 32, Gomes Victor Miguel wa Afrika Kusini miaka 33 na Ibrahim Nourdin wa Misri miaka 36.
  Wengine ni Toure Sekou Ahmed wa Guinea miaka 37, Sadok Selmi wa Tunisia miaka 31, Jackson Pavela wa Namibia miaka 31, Louis Hakizimana wa Rwanda miaka 36, Maguette Ndiaye wa Senegal miaka 29 na Chewe Wisdom wa Zambia miaka 35. 
  Washika vibendera ni Mokrani Gourari wa Algeria miaka 34, Issa Yahya wa Chad miaka 36, Steven Danilek M. Moyo wa Kongo miaka 29, Sosseh Sulayman wa Gambia miaka 36, Sidiki Sidibe wa Guinea miaka 33 na Cheruiyot Gilbert wa Kenya miaka 30.
  Wengine ni Mark Ssonko wa Uganda miaka 37, Warr Adbelrahman wa Mauritania miaka 35, Nabina Blaise Sebutu wa DRC miaka 29, Toure Sengne Cheikh wa Senegal miaka 37, Eldrick Adelaide wa Shelisheli miaka 29, Khumalo Steven wa Afrika Kusini miaka 28, Diakite Moriba wa Mali miaka 37 na Kasengele Romeo wa Zambia miaka 36.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAKUNA REFA HATA MMOJA WA TANZANIA FAINALI ZA U-20 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top