• HABARI MPYA

    Thursday, February 09, 2017

    GRANT ATUPIWA VIRAGO BAADA YA GHANA KUBORONGA AFCON

    SHIRIKISHO la Soka Ghana (GFA) limeachana na kocha wake mkuu, Avram Grant kufuatia Black Stars kushika nafasi ya nne kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka 2017.
    Muisrael huyo ameondolewa kazini licha ya kuiwezesha Black Stars kufika Nusu Fainali ya AFCON kwa mara ya sita mfululizo mwaka huu.
    Taarifa ya GFA imethibitisha kuondoka kwa kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Portsmouth, ambaye mkataba wake ulitarajiwa kumalizika Februari 28, 2017.
    “Mkataba baina ya Shirikisho la Soka Ghana na Abraham Grant unamalizika Februari 28, 2017. Pande zote mbili zimekubaliana kwamba mkataba uwe kama ulivyo. Pande zote zimekubaliana kiungwana kutoongeza mkataba huu ukimalizika,".
    Avram Grant ameondolewa Ghana baada ya Black Stars kushika nafasi ya nne AFCON 2017

    Grant alianza kazi Black Stars Desemba mwaka 2014 na akaiwezesha timu hiyo ya Afrika Magharibi kufika fainali ya AFCON mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea, wakifungwa na Ivory Coast kwa penalti. 
    Mwaka huu wameshika nafasi ya nne baada ya kufungwa 1-0 na Burkina Faso katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu. Wakati huo huo, GFA inasaka kocha mpya wa kufundisha timu yake ya taifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GRANT ATUPIWA VIRAGO BAADA YA GHANA KUBORONGA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top