• HABARI MPYA

  Wednesday, February 15, 2017

  AZAM FC ‘YAWAGIDA’ WANAJESHI WA ZAMBIA 1-0

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeiangusha Red Arrows ya Zambia kwa bao 1-0 usiku huu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Sifa zimuendee beki wa kati, Abdallah Kheri aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 84 kwa kichwa cha kudundisha chini kufuatia mpira wa adhabu wa Khamis Mcha ‘Vialli’.
  Azam FC ilimaliza mchezo huo pungufu, baada ya winga wake Mghana, Enock Atta Agyei kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 89 kufuatia kuonyeshwa kadi za njano mfululizo baada ya kuingia kipindi cha pili.
  Abdallah Kheri akishangilia baada ya kufunga bao hilo pekee dakika ya 84  

  Baada ya dakika 60, Azam walibadilisha kikosi kizima wakiingia Mwadini Ali, David Mwantika, Enock Atta, Samuel Afful, Salum Abubakar, Khamis Mcha, Ismail Gambo, Abdallah Kheri, Gardiel Michael, Masoud Abdallah na Erasto Nyoni.
  Kikosi Cha Azam FC Kikikuwa: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Yakubub Mohammed, Himid Mao, Agrey Morris, Joseph Mahundi, Frank Domayo, Ramadhan Singano, Bruce Kangwa, Yahaya Mohammed Na Shaaban Idd.  
  Kipoindi cha pili; Mwadini Ali, David Mwantika, Enock Atta, Samuel Afful, Salum Abubakar, Khamis Mcha, Ismail Gambo, Abdallah Kheri, Gadiel Michael, Masoud Abdallah Na Erasto Nyoni.
  Red Arrows: Danny Munyao/Kenny Mumba dk59, Jimmy Chisenga/Benedict Chepeshi dk59, Branson Chama, Joseph Zimba/Alex Schone dk59, Webster Mulenga, Stanley Nshimbi, George Simba Yambaya, Bruce Musakanya/Evans Musonda dk63, Lubinda Mundia, Festus Mbewe na Francis Kombe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC ‘YAWAGIDA’ WANAJESHI WA ZAMBIA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top