• HABARI MPYA

    Thursday, November 21, 2013

    SIMBA INATISHA UHAI, YAIFUMUA MGAMBO 5-0 KARUME

    Na Prince Akbar, Ilala
    SIMBA SC imeonyesha ni timu hatari zaidi katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya timu za Ligi Kuu ya Bara, maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya jioni hii kuilaza Mgambo JKT ya Tanga mabao 5-0 Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Ibrahim Hajibu, Issa Abdalla kila mmoja mawili na lingine Miraj Athumani. 
    Katika mchezo wa awali asubuhi, JKT Oljoro ya Arusha iliifunga 1-0 Ruvu Shooting ya Pwani, bao pekee la Salim Bashiri dakika ya 34.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA INATISHA UHAI, YAIFUMUA MGAMBO 5-0 KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top