• HABARI MPYA

  Thursday, February 03, 2022

  SIMBA SC YAIKALISHA PRISONS KWA BAO LA TUTA


  BAO la mshambuliaji Mnyarwanda mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 78, limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, mabingwa watetezi wanafikisha pointi 28 katika mchezo wa 14, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi saba na vinara, Yanga SC ambao pia wana mchezo mmoja mkononi.
  Tanzania Prisons hali inazidi kuwa mbaya baada ya kichapo cha leo, wakibaki na pointi zao 11 baada ya mechi 14 na kuendelea kuzibeba timu nyingine zote 15 kwenye ligi hiyo.
  Katika mchezo uliotangulia, wenyeji, Ruvu Shooting walilazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya Kwanza Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Saadat Mohamed alianza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 36, kabla ya Habib Kyombo kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 51.
  Kwa matokeo hayo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya 14 na Mbeya Kwanza wanatimiza pointi 13, ingawa wanabaki nafasi ya 12 baada ya tlmu zote kucheza mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIKALISHA PRISONS KWA BAO LA TUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top