• HABARI MPYA

  Thursday, February 03, 2022

  AZAM FC YAENDELEA KUTAMBA KATIKA SOKA YA VIJANA


  TIMU ya Azam FC U-20 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano maalum ya vijana (U-20 Tournament 2022), baada ya kuichapa JKT Tanzania U-20 mabao 4-3 usiku wa Jumatano 
  Uwanja wa JMK Park, Dar es Salaam.
  Huo ni ubingwa wa pili kwa kikosi hicho ndani ya miezi miwili, baada ya Desemba mwaka jana kubeba taji la michuano ya Kombe la Chipukizi iliyofanyika jijini Arusha.
  Mabao ya Azam FC U-20 yaliyoipa ubingwa yamewekwa kimiani na Ashraf Malolo dakika ya saba, akimalizia mpira wa kona uliopigwa George Chande.
  Dakika ya 65, Zuberi Mkombozi, alitupatia bao la pili likiwa ni la kusawazisha baada ya JKT kufunga mabao mawili kabla ya kwenda mapumziko kupitia kwa, Vincent Bundala.
  Azam FC U-20 ilijihakikishia ubingwa kwa mabao mengine mawili, yaliyowekwa kimiani na Cyprian Kachwele, aliyeingia kipindi cha pili.
  Kabla ya kutinga fainali Azam FC U-20 ilizichapa Ruvu Shooting (2-1), Magnet Youth (3-1) na kutoka sare na Kepteni (2-2), zikiwa mechi za Kundi A.
  Kwenye hatua ya nusu fainali, Azam FC U-20 ikakutana na Simba na kuitungua bao 1-0, lililofungwa na Jamal Jaku, kabla kuichachafya JKT Tanzania katika fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAENDELEA KUTAMBA KATIKA SOKA YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top