RATIBA ya Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoka na mechi zote za michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitachezwa katikati ya mwezi huu.
Azam FC na Baga Friends watacheza Februari 12 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Yanga SC na Biashara United Februari 15 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mabingwa watetezi, Simba SC watakuwa wageni wa Ruvu Shooting Februari 16 Uwanja wa Mkapa pia.
0 comments:
Post a Comment