• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2019

  SIMON MSUVA AIWEZESHA DIFAA HASSAN EL-JADIDI KUSHINDA 2-1 DHIDI YA MOULOUDIA OUJDA

  Na Mwandishi Wetu, OUJDA 
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana ameisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi kushinda 2-1 dhidi ya Mouloudia Oujda katika mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Manispaa ya Oujda.
  Mabao ya Difaa Hassan El-Jadidi yalifungwa na Elmoustafa Chichane dakika ya 27 na Bilal El Magri dakika ya 85, wakati la Mouloudia Oujda lilifungwa na Milton Karissa dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Difaa Hassan El-Jadidi inafikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 25 na kupanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya sita kwenye msimamo wa Botola Pro inayoshirikisha timu 16.

  Mouloudia Oujda yenyewe inashuka kwa nafasi moja hadi ya saba, ikibaki na pointi zake 32 baada ya kucheza mechi 25 pia katika ligi ambayo, Wydad Casablanca inaongoza kwa pointi zake 52 za mechi 24 ikifuatiwa na Raja Casablanca yenye pointi 43 za mechi 23.
  Kikosi cha Difaa Hassan El-Jadidi kilikuwa; Mohemed El Yousfi, Ettayb Boukhriss, Marouane Hadhoudi, Bakary N'diaye, Youssef Aguerdoum El Idrissi, Ayoub Benchchaoui, Mohammed Ali Bemammer, Anouar Jayid/Adil Elhassnaoui dk65, Simon Happygod Msuva, Bilal El Magri/Julian Nenov dk88 na El Mostafa Chichane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMON MSUVA AIWEZESHA DIFAA HASSAN EL-JADIDI KUSHINDA 2-1 DHIDI YA MOULOUDIA OUJDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top