• HABARI MPYA

  Wednesday, April 17, 2019

  YANGA SC YAPIGWA 1-0 NA MTIBWA SUGAR MECHI YA LIGI KUU LEO MOROGORO

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  MATUMAINI ya ubingwa yamezidi kufifia Yanga SC baada ya kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar mchana wa leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kiboko ya Yanga SC leo alikuwa ni chipukizi Riphat Msuya aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 52 akitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya timu hiyo.
  Na kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 32 na kupandsa hadi nafasi ya nne kutoka ya tano, ikiiteremsha Lipuli FC ya Iringa.

  Riphat Msuya (kushoto) akishangilia na wenzake baada ya kuifungia bao pekee Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga leo

  Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 74 baada ya kucheza mechi 32, lakini baada ya kufungwa mechi ya nne leo inazidi kupoteza matumaini ya ubingwa.
  Inafuatiwa na Azam FC yenye pointi 66 baada ya kushuka uwanjani mara 31 na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 60 kufuatia ushindi wa leo katika mechi ya 23 tu.
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Issa Kajia, Ally Makarani, Salum Kihimbwa, Jaffar Kibaya, Riphat Msuya na Haroun Chanongo.
  Yanga SC; Klaus Kindoki, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Papy Kabamba Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Thabani Kamusoko, Heritier Makambo, Erick Msagati na Raphael Daudi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAPIGWA 1-0 NA MTIBWA SUGAR MECHI YA LIGI KUU LEO MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top