• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 26, 2019

  YAHYA ZAYD ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA 20 ISMAILIA YAPIGWA 3-0 LIGI YA MISRI

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Yahya Zayd jana ametokea benchi dakika 20 za mwisho timu yake, Ismailia ikichapwa mabao 3-0 na Wadi Degla katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Petrosport mjini Cairo.
  Zayd aliyejiunga na timu hiyo msimu huu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam, aliingia uwanjani dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Mohamed Sadek.
  Mabao ya Wadi Degla katika mchezo huo yalifungwa na Hossam Arafat mawili dakika ya 14 na 24 na lingine mshambuliaji Msenegal, Ibrahima Ndiaye dakika ya 65.

  Matokeo hayo yanaifanya Wadi Degla ifikishe pointi 34 baada ya kucheza mechi 29 na kujiinua kutoka nafasi ya 15 hadi 11 kwenye msimamo wa Ligi ya Misri yenye timu 18, wakati Ismailia inabaki nafasi ya saba na pointi zake 37 za mechi 28.
  Mchezo mwingine wa Ligi ya Misri jana, Al Ahly iliichapa Al Masry 2-0 Uwanja wa Border Guard mjini Alexandria, mabao ya Saleh Gomaa dakika ya 31 na  Ali Maaloul kwa penalti dakika ya 73.
  Kwa ushindi huo, Al Ahly inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda nafasi ya pili, ikiishushia nafasi ya tatu Zamalek yenye pointi 60 za mechi 27 pia, wakati Pyramids inaongoza kwa pointi zake 63 za mechi 29.  
  Wachezaji wengine wa Tanzania wanaocheza Misri, viungo Himid Mao wa Petrojet, timu yake inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 34 za mechi 30 za Shiza Kichuya wa ENPPI, timu yake inashika nafasi ya 15 kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 18 ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAHYA ZAYD ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA 20 ISMAILIA YAPIGWA 3-0 LIGI YA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top