• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2019

  EVERTON YAITANDIKA MANCHESTER UNITED 4-0 GOODISON PARK

  Mpira uliopigwa na Richarlison dakika ya 13 ukimpita kipa wa Manchester United, David De Gea kutinga nyavuni kuipatia Everton bao la kwanza katika ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool. Mabao mengine ya Everton yamefungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 28, Lucas Digne dakika ya 56 na Theo Walcott dakika ya 64. Ushindi huo unaifanya Everton ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 35 na kusogea nafasi ya saba, nyuma ya Manchester United inayobaki na pointi zake 64 baada ya kucheza mechi 34 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EVERTON YAITANDIKA MANCHESTER UNITED 4-0 GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top