• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 18, 2019

  CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya marefa 27 na marefa wasaidizi 29 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu nchini Misri, lakini hakuna Mtanzania hata mmoja.
  Waamuzi hao wameteuliwa kushiriki kozi maalum kuanzia Aprili 28 hadi Mei 5 mwaka huu mjini Rabat, Morocco kunolewa kwa ajili ya Fainali za Misri mwezi Juni.
  Marefa hao wanatoka nchi 33 na wataingia kwenye kambi maalum ya mafunzo itakayosaidia uteuzi wa orodha ya mwisho ya marefa watakaochezesha fainali za mwaka huu zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19 katika miji ya Alexandria, Cairo, Ismailia na Suez.
  Florentina Zabron, mmoja wa marefa waliochezesha mechi nyingi msimu huu Tanzania

  Wakiwa mjini Rabat, kwanza marefa hao watafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kufanyishwa mtihani wa utimamu wa miili chini uya usimamizi wa wakufunzi wazoefu wa CAF. 
  Baada ya hapo wataingia darasani kwa majadiliano ya sheria za mchezo, ambayo yataanza Juni 1 ambazo zitakwenda kutumika kwenye michuano hiyo.
  Misri na Tunisia zimeongoeza kwa kutoa marefa wengi AFCON 2019, watano kila nchi, watatu wapuliza filimbi na wawili washika vibendera.
  Marefa walioteuliwana nchi zao kwenye mabao ni Mustapha Ghorbal (Algeria), 2 Helder Martins De Carvalho (Angola), Joshua Bondo (Botswana), Pacifique Ndabihawenimana (Burundi), Alioum Alioum (Cameroon), Amin Mohamed Omar (Misri), Gehad Gerisha (Misri), Mahmoud Zakria El Banna (Misri), Bamlak Tessema (Ethiopia) na Eric Arnaud Otogo Castane (Gabon).
  Wengine ni Gassama Bakary Papa (Gambia), Daniel Nii Ayi Laryea (Ghana), Peter Waweru (Kenya), Mahamadou Keita (Mali), Redouane Jiyed (Morocco), Noureddine El Jaafari (Morocco), Jackson Pavaza (Namibia), Jean-Jacques Ndala Ngambo (DRC), Louis Hakizimana (Rwanda), Maguette Ndiaye (Senegal), Bernard Camille (Shelisheli), El Fadil Mohamed Hussein (Sudan), Victor Miguel De Freitas (Afrika Kusini), 27 Janny Sikazwe (Zambia), Sadok Selmi, Youssef Essrayri na Guirat Haythem wote wa Tunisia. 
  Marefa wasaidizi ni Mokrane Gourari (Algeria), Abdelhak Etchiali (Algeria), Jerson Emiliano Dos Santos (Angola), Seydou Tiama (Burkina Faso), Nguegoue Elvis Guy Noupue (Cameroon), Evarist Menkouande (Cameroon), Issa Yaya (Chad), Soulaimane Almadine (Comoro), Tahssen Abo El Sadat (Misri), Abouelregal Mahmoud (Misri), Tesfagiorghis Berhe (Eritrea), Samuel Temesgin (Ethiopia), Sidibe Sidiki (Guinea), Gilbert Cheruiyot (Kenya) na Souru Phatsoane (Lesotho).
  Wengine ni Attia Amsaaed (Libya), Lionel Andrianantenaina (Madagascar), Azgaou Lahcen (Morocco), Arsenio Maringule (Msumbiji), Mahamadou Yahaya (Niger), Baba Adel (Nigeria), Oliver Safari (DRC), El Hadji Malick Samba (Senegal), Djibril Camara (Senegal), Zakhele Thusi Siwela (Afrika Kusini), Mohammed Ibrahim (Sudan), Waleed Ahmed Ali (Sudan), Yamen Mellouchi na Anouar Hmila wote wa Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top