• HABARI MPYA

  Thursday, April 18, 2019

  DK MSOLLA NJIA NYEUPE UENYEKITI YANGA SC BAADA YA LUCAS MASHAURI KUJITOA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Dk Mshindo Msolla atapambana na Elias Mwanjala, Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga kuwania Uenyekiti wa klabu ya Yanga katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam.
  Hiyo ni baada ya Lucas Mashauri aliyekuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda kuenguliwa kutokana na kutojitokeza kwenye usaili.
  Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga inayoshirikiana na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamepitishwa wagombea wawili wapya.

  Dk Mshindo Msolla atapambana na Elias Mwanjala pekee kuwania Uenyekiti wa Yanga Mei 5

  Hao ni Katibu wa zamani wa TFF, Frederick Wilfred Mwakalebela na Mbunge wa jimbo Ileje (CCM) Mheshimiwa, Janet Zebedayo Mbena baada ya Samuel Lukumay na Thobias Lingalangala kuenguliwa kwa pingamizi.
  Hao wanaungana na Yono Kevela, Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota waliopitishwa awali kabla ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
  Taarifa hiyo iliyosainiwa na Wenyekiti wote wa Kamati za Uchaguzi, Mawakili Malangwe Mchungahela wa TFF na Sam Mapande wa Yanga imesema kwamba wagombea tisa wapya wamepitishwa kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.
  Hao ni Dominick Albinus, Saad Mohamed Khimji, Hassan Yahya Hussein, Shafiru Amour Makosa, Mhandsi Bahati Faison Mwaseba, Hamad Ali Islam, Mhandisi Leonard Marangu, Suma Mwaitenda na Haruna Hussein Batenga. 
  Hao wanaungana na wengine 16 waliopitishwa awali ambao ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.  
  Na hiyo ni baada ya wagombea wengine kujitoa, ama kuenguliwa kwa mapingamizi au kutokukidhi vigezo baada ya usaili jana wakiwemo Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.
  Wengine waliojiuzulu katika uongozi wa Yanga uliongia madarakani Juni 11 mwaka ni aliyekuwa Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wanne, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DK MSOLLA NJIA NYEUPE UENYEKITI YANGA SC BAADA YA LUCAS MASHAURI KUJITOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top