• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 25, 2019

  MICHUANO YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 NA U15 YAENDESHWA NCHI NZIMA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MICHUAO ya Ligi ya Wilaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 15 (U15) na U17 inaendelea katika wilaya mbalimbali za Tanzania.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amewaambia Waandishi wa Habari leo katika taarifa yake kwamba ligi hizo zinaendelea vizuri.
  Ndimbo amesema kwamba kuanzishwa kwa Ligi hizo kuanzia ngazi ya chini ni juhudi za TFF katika harakati zake za kuendelea kuwekeza katika Soka la Vijana.

  Amesema kwamba ligi hiyo katika ngazi ya Wilaya inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili na kufuatiwa na Ligi ya Vijana U15 na U17 ngazi ya Mkoa mwezi Mei, kabla ya Ngazi ya Taifa kufuatia Juni, mwaka huu.
  Ndimbo amesema kwamba TFF inaendelea kuwekeza katika Soka la Vijana ambako ndiko kwenye msingi wa maendeleo ya Mpira wa Miguu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MICHUANO YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 NA U15 YAENDESHWA NCHI NZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top