• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2019

  NIGERIA, CAMEROON ZATINGA NUSU FAINALI AFCON U17

  TIMU ya taifa ya Guinea imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Morocco jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Hongera zake mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Momo Fanye Toure dakika ya 64 na kwa ushindi huo, Guinea inakamilisha mechi zake za Kundi B na pointi sita, ikizidiwa moja na Cameroon iliyoongoza na zote zinafuzu Nusu Fainali.
  Mchezo mwingine wa mwisho wa kundi hilo leo, Cameroon imetoa sare ya 0-0 na Senegal Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 

  Cameroon itamenyana na mshindi wa pili wa Kundi A, Angola katika Nusu Fainali Jumatano, wakati Guinea itamenyana na vinara wa kundi hilo, Nigeria siku hiyo pia Uwanja wa Taifa.
  Nigeria, Cameroon, Guinea na Angola zimekata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Brazil, wakati Morocco na Senegal zinaungana na Uganda na Tanzania kutoka Kundi A kuaga michuano hiyo mapema tu baada ya hatua ya makundi. 
  Ikumbukwe, bingwa mtetezi, Mali hakufuzu kwenye fainali za mwaka huu zitakazofikia tamati Jumapili kwa mchezo wa fainali Uwanja wa Taifa, siku moja baada ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIGERIA, CAMEROON ZATINGA NUSU FAINALI AFCON U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top