• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2019

  SERENGETI BOYS YA KWANZA KUFUZU AFCON U17 KIHISOTRIA 2005 GAMBIA

  Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kabla ya mchezo wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U17) dhidi ya Zimbabwe Januari 8, mwaka 2005 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam. Serengeti Boys ilishinda 3-1 Zimbabwe na ikaenda kushinda pia 1-0 Bulawayo kwenye mchezo wa marudiano na kufuzu fainali hizo zilizofanyika Gambia mwaka huo, ingawa haikwenda kushiriki baada ya kuenguliwa kwa kashfa ya kutumia mchezaji aliyezidi umri, Nurdin Bakari. 
  Waliosimama kutoka kulia ni Kocha Mkuu, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, Jumanne Ramadhani, Yusuph Mgwao, Juma Jabu, Nurdin Bakali, Athumani Iddi ‘Chuji’, Patrick Mangunguru na Kocha Msaidizi, Sylvester Marsh (sasa marehemu).
  Waliochuchumaa kutoka kulia ni Julius Mrope, Nizar Khalfan, Omar Matuta, Hamad Haidari na Nahodha, Ally Milungo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YA KWANZA KUFUZU AFCON U17 KIHISOTRIA 2005 GAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top