• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2019

  SERENGETI BOYS NA NIGERIA KATIKA PICHA UFUNGUZI AFCON U17 JANA

  Mshambuliaji wa Tanzania, Edmund John akimtoka beki wa Nigeria katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Nigeria ilishinda 5-4.
  Edson Mshirakandi wa Serengeti Boys akiupigia hesabu mpira wa juu
  Arafat Swalaki wa Serengeti Boys (kulia) akijaribu kuzuia shuti la mchezaji wa Nigeria
  Kiungo wa Nigeria, Akinkunmi Amoo akijaribu kupasua katikati ya wachezaji wa Tanzania
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akimsabahi mchezaji wa Nigeria kabla ya mchezo na Serengeti Boys
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa michuano jana 
  Rais wa CAF, Ahmad akihutubia wapenzi wa soka jana Uwanja wa Taifa 
  Shabiki wa Tanzania akipeperusha bendera jana Uwanja wa Taifa 
  Msanii chipukizi wa kike akitumbuiza jana Uwanja wa Taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa michuano ya AFCON U17
  Wasaniiwakitumbuiza jana Uwanja wa Taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa michuano ya AFCON U17
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS NA NIGERIA KATIKA PICHA UFUNGUZI AFCON U17 JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top