• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 14, 2019

  YAKUBU AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE LIGI KUU LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Shukrani kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mghana Yakubu Mohamed dakika ya 45 na ushei na kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya Yanga yenye pointi 74 za mechi 31 pia.
  Mabingwa watetezi, Simba SC wanafuatia katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 22, kutokana na kutingwa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Lakini baada ya kutolewa katika hatua ya Robo Fainali kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa TP Mazembe jana mjini Lubumbashi, Simba SC itakuwa na mechi mfululizo kumaliza viporo vyake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAKUBU AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE LIGI KUU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top