• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 18, 2019

  SPURS YAITUPA NJE MAN CITY LIGI YA MABINGWA ULAYA

  Wachezaji wa Tottenham Hotspur wakishangilia mbele ya mashabiki wao waliosafiri kuwafuata Uwanja wa Etihad mjini Manchester jana wakimenyana na wenyeji, Manchester City katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Manchester City ilishinda 4-3 na kufanya sare ya jumla ya 4-4 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Tottenham na kwa maana hiyo, Spurs wanakwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao mengi waliyofunga ugenini na watamenyana na Ajax iliyoitoa Juventus. Mabao ya Tottenham yalifungwa na Son Heung-Min dakika ya saba na 10 na Fernando Llorente dakika ya 73 kwa msaada ya Picha za Marudio ya Video (VAR), wakati ya Manchester yalifungwa na Raheem Sterling mawili dakika ya nne na 21, Bernardo Silva dakika ya 11 na Sergio Agüero dakika ya 59. Sterling angeondoka na mpira jana na kuipeleka Man City Nusu Fainali kama bao lake la dakika za majeruhi lisingekataliwa na VAR 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPURS YAITUPA NJE MAN CITY LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top